Abstract:
Makala hii inachunguza mkakati wa tafsiri mkopo wa istilahi za
Kiingereza katika Kiswahili na athari zake kwa kuangazia uga wa
biolojia, fizikia na kemia kupitia vidahizo teule vya Kamusi ya
Biolojia, Fizikia na kemia (2012). Azma kuu ya uchunguzi huu ni
kutathmini mchango wa tafsiri mkopo wa msamiati wa Kiingereza
katika suala zima la kukuza lugha ya Kiswahili. Kwa mujibu wa
makala hii eneo hili halijapewa aula miongoni mwa mada
mbalimbali za tafsiri zilizokwishachunguzwa. Hii
imemuhamasisha mtafiti kulishughulikia eneo hili. Data ya makala
hii ilikusanywa uwandani katika idara na taasisi zilizo katika jiji la
Dar es Salaam kwa njia ya usaili, hojaji na chanzo cha data cha
maktabani. Idara na taasisi zilizohusishwa katika ukusanyaji wa
data ni: Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu, TATAKI kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na BAKIZA. Idara na taasisi hizi
zinapatikana mkoani Dar es Salaam Wilaya ya Ubungo ambapo
mtafiti alifanikiwa kudodosa na kufanya mahojiano ya ana kwa ana
kwa wataalamu wa tafsiri. Aidha, data ilikusanywa kutoka katika
matini mbalimbali kutoka chanzo cha data cha maktabani.
Mathalani, kamusi, tasinifu, majarida na vitabu kadhaa kulingana
na mada ya makala hii. Malengo ya makala hii yametimizwa kwa
kuongozwa na Nadharia ya Istilahi za Kisayansi iliyoasisiwa na
Kiingi (1989) na kuendelezwa na Kiingi (1992) na Kiingi (1998) na
Mwaro-Were (2000, 2001). Halikadhalika, data ya makala hii
imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa maelezo. Aidha,
matokeo yameonesha kuwa Kiswahili kimejipatia istilahi lukuki
katika tasnia ya biolojia, fizikia pamoja na kemia kupitia mkakati wa
tafsiri mkopo. Makala hii ni muhimu kwa wanaisimu kwani
inabainisha istilahi mbalimbali za lugha ya Kiingereza katika uwanja
wa biolojia, fizikia pamoja na kemia zilizoingizwa katika Kiswahili
kupitia tafsiri mkopo. Inapendekezwa kuwa watafiti wa lugha